MAKALA KUHUSU MINYOO KWA KUKU

IMEANDALIWA NA 

 Greyson kahise

 Mtaalamu wa kuku

 0769799728

 0715894582



👉Minyoo ni viumbe hai ambao huishi kwa kutegemea uwepo wa kiumbe mwingine kwa malazi na chakula

👉Kwa kuku minyoo ipo ya aina nyingi, ipo ile ya duara, ipo ile inayokua mirefu sana ambayo ikiwapata kuku kupotea huchukua muda mrefu

CHANZO CHA MINYOO

👉Kuku kula chakula kichafu hasa kilicho changanyika na kinyesi...hapa hasa kama unachanganya kuku wakubwa na wadogo madhara huwa endelevu bandani usipokinga

👉Kuku wanao zunguka nje, kunywa maji yaliyotuama au maji yaliyokaa kwa muda mrefu pia kuparua mabaki yenye mazalia au mayai ya minyoo

👉Kwa kawaida minyoo huwa na mzunguko wao kunzia *YAI, LAVA, PUPA ,NA MNYOO* mnyoo mkubwa...hivyo minyoo ikiingia kwa kuku huvhukua muda wa wiki zaidi ya mbili kukua kufikia mnyoo kamili

👉Kuku akishapata minyoo wakubwa...hapa ndipo tatizo huanzia kwani mahai hutagwa kwa wingi na hutolewa kwa njia ya kinyesi na kuwafikia kuku wengine hivyo kama hatua za maksudi hazitachukuliwa ndani ya muda wa wiki 4 tangu minyoo kuingia bandani asilimia kubwa ya kuku watakua na minyoo

KUZUIA

👉Hakikisha mazingira yako ni salama na safi muda wote yasiyo na maji yenye kutuama kwa wala matope yanayo kuwepo kwa muda wote kuzunguka mahali kuku wanapoishi

TIBA

👉Kitaalamu zipo dawa nyingi za minyoo ambazo kwa ratiba iliyo zoeleka hutakiwa kutolewa na kurudiwa kila baada ya miezi mitatu

👉Tatizo limekuja ni upi wakati sahihi wa kuanza dozi ya minyoo  kwa kuuliza madaktari bobezi wa kuku wanashauri dawa za awali za minyoo zitolewe baada ya miezi miwili

INASHAURIWA KWA SEHEMU ZENYE MAJI YASIYO SALAMA SANA

👉Na mfumo wa utoaji dawa za minyoo kwa Mara ya kwanza unatakiwa uwe wa kurudia kila baada ya wiki 2 rudia Mara tatu

KWA NINI IRUDIWE UNAPOANZA DOZI

👉Dawa za minyoo hushambulia hatua mbili za ukuaji wa minyoo..ambazo ni minyoo wakubwa na wale wanaofuata kwa ukubwa ilaa haziathiri hatua za mayai na LAVA...hivyo ukiwapa dawa kwa kurudia kila baada ya wiki mbili  Mara  3 mfululizo hii itapelekea hata yale mayai yatakua yamegeuka na kuwa  minyoo wakubwa hivyo dawa itawaua na kupunguza tatizo kwa 75-85%

👉Ila ukiwa unasubiri kuwapa kila baada ya miezi mitatu bila kufanya hizo hatua nilizolekeza utakua unapunguza idadi ya minyoo na wakati mwingine minyoo itazidi na haitasikia dawa



Zipo dawa aina nyingi za minyoo kama Ant worms ...Piperezine...,Levamisole, Leva,Askarex , Fenhbendazole .zipo nyingi sana madukani 

 KWA URAHISI

👉Awamu ya kwanza ya kuwapa dawa

👉Baada ya miezi miwili....dozi siku 1-2

👉Rudia baada ya wiki 2 dozi siku 1-2

👉Rudia baada ya wiki 2 dozi siku 1-2

Ukimaliza hapo sasa wape dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu kuku wako watakua salama na huru dhidi ya minyoo

ZINGATIA

👉Maji safi

👉Chakula safi

👉Banda safi

👉Fuata ratiba sahihi ya dawa hasa kila baada ya miezi mitatu zingatia usipitishe na uzipuuze

BILA SHAKA TUMEELEWANA

Asante Kwa kusoma .

Nauza Formula 20000

Kitabu 10000

Nauza vifaranga Aina zote