*SOMO GUMU LA KUKU NA UCHUMI*


👉Je ni KWANINI upoteze *milioni 7* kwasababu ya kuikwepa *laki 2 au 3???*

Naanza kufundisha Kwa mifano ili tuelewane kidogo.....Kwa makaridio kuku mmoja wa mayai tangu kifaranga mpaka kuwa kuku wa kutaga anaweza kugharimu Kati ya *12000-14000*

Hivo kwa mfugaji anaefuga kuku *500* anatumia wastani wa milioni *6-7* kuwakuza kuku wake mpaka waanze kutaga.

Gharama za kuhudumia hawa kuku zinaweza kupanda zaidi iwapo kuku wataugua na *utatumia pesa nyingi kununua madawa*

👉Ikumbukwe wafugaji wengi tunahofia Sana gharama ndogo zunazoweza kusababisha gharama kubwa baadae ( *Cheap is expensive)*

Mfano: Mfugaji yupo tayali kuhudumia mradi wake wa kuku 300 kupitia kutuma jumbe kwenye group za *WhatsApp au FB*  manaake huyu haoni kabisa haja ya kuwa na dakatari au mtaalamu mshauri kwakukwepa *gharama isiyozidi pengine hata laki 1 Kwa miezi mitani*

👉Madhara yake ninini , mfugaji anajikuta kutumia gharama kubwa kununua madawa ya Aina tofauti tofauti, mfugaji anapoteza kuku wake wengi pengine hata kukata tamaa na hapo *anakua amepoteza zaidi ya milioni 3 Kwa kuikwepa gharama ya mtaalamu ya laki 1.*

Hapo nimeongelea kuhusu mauzo ya kuku pekee na sijapeleka kwenye tathmini ya mayai ambayo yangetagwa na hawa kuku

Kwahiyo kama utapoteza kuku 300 wa mayai ni wastani wa mayai *tray 7- 8* Kwa siku ...ambayo thamani yake Kwa siku ni zaidi ya *50000* ...ambayo thamani yake Kwa Mwezi ni zaidi ya *milioni moja na nusu.*



 *NAWAIBIA SIRI KIDOGO*

👉Tumeshawahi kujiuliza KWANINI wenye *miradi mikubwa huajiri wataalamu wa fani Husika???* na nikwanini pamoja na kwamba walioajiriwa wanataaluma lakini bado *huwapeleka kwenye mafunzo ya mara Kwa mara* 

JIBU: Ufugaji kibishara unahitaji utaalamu na ujuzi WA Mambo, ambayo hubadilika *kutokana na Mabadiliko ya kiteknolojia*  Hivo kuna haja kubwa Sana Kwa wafugaji *KUBADILIKA KIMTAZAMO KUKUBALI KUACHA MAZOEA NA KUELEKEA NJIA SAHIHI YA MATUMAINI*

👉Ipo hivi, binafsi nimfugaji mdogo Sana lakini nafuga Kitaalamu changamoto hazikosekani Ila nazipunguza Kwa kiasi kikubwa, *NILISIMAMIA* Shamba kubwa lenye kuku zaidi ya *30000* lakini Kunakua na Sheria na mipango madhubuti *kuhakikisha kuku wanakua salama kwanza, kisha kuhakikisha uzalishaji unakua juu.* 

NGUZO KUU ZA KUFIKIA MALENGO YA UFUGAJI KUKU KIBIASHARA

👉Ratiba sahihi ya *chanjo* na *dawa za minyoo* inayo fuatwa kiusahihi bila kupepesa macho

👉Mpangilio sahihi wa chakula kutokana na umri wa kuku bila kukosea.

👉Vipimo vya mara kwa mara vya kuku ili kubaini afya zao ( *USITIBU KUKU KWA KUBASHIRI UGONJWA* ).

👉Kutumia wataalamu wa Kada Husika 

👉Kuzalisha bidhaa Bora sokoni , Hapa ndipo utakua na uhakika wa kuuza bidhaa zako za kuku.

👉Kwa wafugaji wadogo kupata soko kubwa inapaswa kuunganisha nguvu za pamoja.

 *💯HAYO NI BAADHI YA MAMBO MUHIMU SANA YA KUZINGATIA*

Nimalizie Kwa kusema kwamba 

👉Ufugaji wa kuku ni kazi kama kazi nyingine kama unatakiwa kufuga KIBIASHARA nilazima ukubali Kugharamia vitu mbalimbali *MIMI KAHISE* sipo Hapa kukupa Tu moyo kwamba ufuge utapata mafanikio wakati hutataka Kugharamia *CHANJO* , *utaalamu* Vipim n.k NILAZIMA Kwanza tubadilishe mtazamo kisha tutaona matunda kwenye Ufugaji.

MWISHO TUWE WAVUMILIVU NA KUKUBALI MABADILIKO YA KIMFUMO 

Asanteni Sana 

Karibu Kwa swali au maoni kuhusu SOMO HILI