*SOMO LA KWANZA 2022*

 *CHANGAMOTO KUU ZA MRADI WA KUKU NA NAMNA YA KUZITATUA* 
Imeandaliwa na 
 *Greyson Kahise* 
 *Mtaalamu wa kuku* 
 *_0769799728_* 
 *_0715894582_*

🖊️ *KNOWLEDGE/UELEWA/TAALUMA*
☝️Mradi wowote unapo anzishwa unahitaji Utaalamu halisi kuhusu mradi husika,, unaweza ukawa na Mtaji ukapotea Kwa KUANZISHA MIRADI bila kuwa na utaalamu sahihi *SULUHU* Kabla ya *KUANZISHA* mradi WA kuku tafuta *TAALUMA* ya Ufugaji Kwa Vitabu, Semina au *Ajiri mtaalamu* awe karibu kukuongoza kwenye mradi wako.

🖊️ *CAPITAL/MTAJI*
☝️Mradi WA kuku kibiashara sio maigizo, unahitaji uwekezaji wenye mlengo wa kibiashara Pasipo kujaribu, *Mfn* : Gharama za Mwanzo za Ujenzi wa mabanda huwa ni Kubwa, na Gharama za kuendesha mradi pia huwepo Kwa kupanda au kushuka Kwa maeneo tofauti.
 *SULUHU*: Ili Kufanya mradi endelevu ambao hautakwama, Nivema mfugaji Ufanye tathmini ya jumla ya mradi unaopanga KUANZISHA ili ujipange taratibu namna sahihi ya kuanza *Kwa kuangalia chanzo cha Fedha ya kuanzishia mradi wako.*

🖊️ *MARKET/SOKO*
☝️Biashara ya kuku ni Huru Kwa maeneo yetu mengi Nchini, Kwa Hali hii hupelekea wafugaji kukutana na changamoto za *Mauzo ya Kuku, Mayai au nyama wakati mwingine* Kwa kutambua Hilo NI vema Sana kabla ya kuamua Aina Fulani ya kuku WA kufugwa Ufanye yafuatayi
 *SULUHU*: Tambua unapo fugia ni *Aina* ipi ya bidhaa inahitajika Kwa wingi, *Ninani* hasa atakua Mteja wako wa moja Kwa moja, *Umoja* wa kimauzo husaidia kuweza kukidhi mahitaji ya *soko* kuliko kuuza ukiwa mmoja mmoja. *Zalisha* bidhaa Bora shindani Sokoni, Ongeza thamani yaBidhaa ( *Kuchinja, Kupark kwenye vifungashio, Kufanya delivery n.k).*

🖊️ *RECORD KEEPING/UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU*
☝️Miradi mingi hasa midogo imekua Shida Sana kuendelea Kwa sababu hakuna utaratibu sahihi wa kutunza kumbukumbu mashambani, Hii hupelekea uhaba WA taarifa za maendeleo ya mradi hivo huwa Ngumu Kwa mfugaji Kufanya tathmini ya moja Kwa moja iwapo mradi unatija au hauna tija
 *SULUHU* Viandaliwe Vitabu vya kumbukumbu mashambani , au Komputer au Application online za kusaidia kutunza kumbukumbu ili kujipima Kwa namna gani mradi unakua na pia unaonekana kujiendesha.

🖊️ *DISEASES/MAGONJWA*
☝️Hapa ndipo wafugaji wengi wanapo kuja kukata tamaa ya Ufugaji, Magonjwa hupelekea kuku Kufa, wengi , au wote bandani, Magonjwa hupelekea Ukuaji kuwa Mbovu, Magonjwa husababisha Kuku kupunguza uzalishaji Kwa kiasi kikubwa Sana 
 *SULUHU* 
☝️Dhibiti magonjwa Kwa kujiwekea taratibu za kufuata ( USAFI USAFI USAFI ) wa kila kitu shambani iwe ni kipaumbele cha Kwanza kuzuia magonjwa ya mara Kwa mara.
☝️ *Biosecurity* Jiwekee sheria za kufuata , Mavazi maalumu, Viatu maalumu, asiingie kila MTU bandani, Mizoga iteketezwe mbali na Banda, Chakula Safi, Banda Bora na sahihi, Usichanganye mifugo mingi eneo moja n.k Kwa namna hii itasaidia Sana kupunguza magonjwa
 *NB!* *CHANJO NI MUHIMU ZAIDI KUZINGATIA KATIKA KUHAKIKISHA MAGONJWA YANAPUNGUA KWA ASILIMIA KUBWA SHAMBANI KWAKO*

🖊️ *SOURCE/VYANZO ( Chakula na Vifaranga)*
☝️Ni Bora kutumia chakula Bora cha gharama kikakupa matokeo kuliko kutumia chakula kisicho Bora cha gharama nafuu kikakupa harasa ( *CHEAP IS EXPENSIVE).*
☝️Nunua Chakula, au Vifaranga kutoka Kwa wazalishaji wanao aminika kiubora ili kuongeza tija kwenye mradi wako.

🖊️ *MAZINGIRA/ENVIRONMENT FORCE*
☝️Tutakua mashahidi kuna msimu ( Baridi au joto) Kuku Ukuaji husumbua, Utagaji hushuka Sana 
🤝Ni vema kuzibaini nyakati hizi ndani ya eneo ulipo na utafute taarifa sahihi za namna ya Kupambana na haya Mabadiliko ya kimazingira ili Ufugaji wetu uendelee kuwa na tija.

🖊️ *UPANDAJI WA BEI ZA VYAKULA NA VIFARANGA* 
☝️Kuna nyakati vifaranga huwa adimu hivo uhitaji huzidi uzalishaji Kwa namna hii BEI za kununua vifaranga hupanda Sana ( *NIMUHIMU* nyakati kama hizi wafugaji kuwa wamoja na kuhakikisha Mauzo ( *BEI ZA Bidhaa Sokoni ziendane na Gharama za uzalishaji)* 
☝️Chakula Kwa wale wanaojitengenezea ni vema kukusanya Akiba ya malighafi za Kutengeneza chakula kipindi BEI zake ni za kawaida hii husaidia Sana Pindi zinapo kuja kuongezeka Kwa ghafla.

 *ZIPO CHANGAMOTO NYINGI Tutaendelea Kukumbushana Ila Hizi zianze kufungua njia na UELEWA WA namna ya Kupambana nazo .*

KARIBU *KAHISE POULTRY SOLUTIONS* FAHARI YA MFUGAJI
🐓🐓🐓🐔🐣🐤🐓🐓🐓🐓🐓