HINTS/ NUKUU ZA NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA YA KUKU
Mawasiliano
Jina Greyson Kahise Mtaalamu wa Kuku
0715894582
0769799728
Email : kahisegreyson81@gmail.com
🤝Leo napenda tupate kukumbushana juu ya namna ambavyo tunaweza kuzuia Magonjwa mbalimbali nyemelezi Kwa kuku shambani.
Kitu kikubwa na cha muhimu zaidi cha kuzingatia ni USAFI wa Banda , USAFI wa maji, USAFI wa chakula, USAFI wa mazingira yanayo zunguka Banda.
Nitaandika Magonjwa kadhaa moja baada ya jingine hatua Kwa hatua nini ufanye.
MOJA: Coccidiosis au kuhara damu.
👉Huu ni ugonjwa ambao umekua ukisumbua Sana kuku wa rika zote, wadogo na hata wakubwa
*Husababishwa na Protozoa Coccidia*
👉Mazingira sababishi ya ugonjwa huu, ni Banda lenye unyevu au Randa zilizo loana muda mwingi.
👆 *Suluhu kubwa* tukiachana na dawa: Hakikisha kuku wako wanaishi pakavu
👆Badilisha Randa zilizo loana na kuweka randa kavu
👆Weka vyombo vya maji juu kidogo ili kuku wasimwage mwage maji bandani.
*MBILI:* *TYPHOID/SALMONELLA*
👉Huu ni ugonjwa mbaya na Hatari Kwa kuku hutokea Kwa kuku rika zote.
Ugonjwa huu huweza kuhama kutoka kwa kuku mzazi kwenda Kwa kifaranga kupitia yai, na kifaranga huupata na kuonesha dalili mapema baada ya kuanguliwa unaitwa ( *Pollurm Kwa vifaranga).*
👉Ugonjwa huu huua taratibu taratibu Ila Vifo vinakua haviishi bandani, Kuku hukonda, Huharisha nyeupe, pia kuku hawa hukonda saana mfupa WA kifua na kupoteza Sana Uzito.
*Suluhu* Pata vifaranga kutoka mashamba yasiyo na shambulio na ugonjwa huu Kwa kuku wazazi
Wape chakula na maji masafi
Safisha Banda ipasavyo hasa baada ya kujua kuwa ugonjwa huu ulitokea awali,
*NB: Ugonjwa huu hautibiki 100% hupona baada ya muda huibuka tena .*
Kuna chanjo ya Typhoid ukiipata itakufaa zaidi.
*TATU:* *MAFUA MAKALI NA A VITAMINOSIS* ( Upungufu wa *Vitamin A)*
Dalili za Magonjwa haya huendana au hushabiiana ili kutofautisha kiusahihi mtumie Daktari)
Mazingira sababishi
👈 UPUNGUFU WA VITAMIN A
👆Kuku kutopewa vitamin hasa vifaranga
Suluhu,vifaranga wako na kuku wakubwa wapewe vitamin na majani mara kwa mara husaidia kuondoa tatizo.
MAFUA MAKALI/Infections Coryza
👉Huu ni ugonjwa hatari na unaoua Sana Kwa sasa hasa kuku wa chini ya miezi 3.
👉Tumekua tukijaribu namna Mbali Mbali kupambana na ugonjwa huu Kwa madawa na Kwa kuijaribu kuweka mazingira usijitokeze.
FANYA YAFUATAYO
👈Pata kinga/ chanjo ya ugonjwa huu kama utafanikiwa.
👈Jenga Banda linaroruhusu hewa kuingia na kutoka
👈Zuia kutumia maranda yenye vumbi kiwango kikubwa, badala yake andaa Randa walau wiki mbili kabla ya kufika kuku ili vumbi na harufu Kali vipungue.
👉Weka kawaida walau kila jioni kuingia bandani kusikiliza uhemaji, ukohoaji WA KUKU wako, pindi usikiapo dalili za chafya au kikohozi ni Bora ukaanza kuwatibu mapema kabla Hali haijawa mbaya.
NNE:NDUI ( FOWL POX).
👉Huu ni ugonjwa wa virusi na huwapata kuku wa rika zote, na hivi karibuni kwa baadhi ya maeneo umekua ukijitokeza mapema wiki ya 2_3 na kupeleka vifaranga kupata vinundu vinundu ( Machoni, mdomoni, miguuni , mgongoni na maeneo mengine yasiyo na ngozi).
MAZINGIRA SABABISHI
👉Kuchanganya Aina tofauti za Ndege mfano, Bata na kuku , Kuku wa kienyeji na wakisasa n.k.
Ni vema Sana Aina moja ya kuku ifugwe kwenye
Banda moja
KUKINGA
👉Kuku wako wachanjwe chanjo ya Ndui ( ya Bawa, au hii Mpya ya matone). Hasa kuanzia wiki ya 4 au 5 japo maeneo mengine inacheleweshwa na mengine inawahi zaidi.
HUDUMA KWA ALIEPATA UGONJWA
👉Atengwe kundini na kuku wazima
👉Safisha vidonda , au vinundu alivyonavyo, mpake mafuta ya kula, au Iodine vitakauka.
👉Mwisho kabisa wape dawa OTC Broad spectrum itawaponesha.
👉Kama hukuwa umewachanja wakipona wachanje chanjo ya NDUI.
Nimeandika nukuu fupi zinazoweza kumsaidia mfugaji mfuatiliaji wa mambo kupunguza Vifo visivyo vya lazima sana
KWA SWALI, MAONI, USHAURI, NA NYONGEZA YA SOMO USISITE KUNIAMBIA
Asante sana


0 Comments