*MAMBO YASIYO PEWA KIPAUMBELE NA WAFUGAJI WA KUKU, AMBAYO HUWAGHARIMU KWA KIASI KIKUBWA.*
Imeandikwa na
*Greyson Kahise*
Mtaalamu wa kuku
0769799728
0715894582
☝️Leo naomba tuangazie mambo kadhaa ambayo wafugaji wengi wamekua wakifanya Pasipo usahihi, ama baada ya kuona madhara ya kuku Kufa n.k
*Moja* : *KUKATA MIDOMO/ DE-BEACKING*
☝️Kuku kukatwa midomo Sio sheria kufanyika iwapo kuku wako watapewa chakula na matunzo yote sahihi, na wanaweza kukua Pasipo Kula mayai au Kudonoana
👉Ila kujihakikishia usalama na ustawi WA kuku wako ( *Mayai au Chotara, Kuku wa asili* ), huwa inashauriwa kuku kukatwa midomo
👉Muda unao shauriwa NI wakiwa na Umri Kati ya wiki *8, au 12, au 16* Hakikisha kuku wako kabla hawajaanza kutaga wameshakatwa midomo ili *Stress* isiwarudishe nyuma kuanza kutaga *NB Zoezi hili lifanywe na Daktari au mzoefu kuzuia umwagikaji wa Damu Kwa hawa kuku na wengine wameshuhudia kuku wakikatwa ulimi na Kufa.*
*MBILI: UWEKAJI WA VIOTA VYA KUTAGIA BANDANI/ NEST BOXES*
☝️ Ifahamike kuku wanaoandaliwa kutaga hutakiwa kuandaliwa mazingira ya kutagia mapema ili wazoee
👉Kuku anahitaji sehemu yenye Giza kiasi ili atage Kwa uhuru ,hivo NI vema kiota utakacho tengeneza kiwe kina Giza kiasi.
👉Muda sahihi wa kuingiza viota bandani ni Kati ya *wiki ya 10-16* , kutegemea Aina ya kuku unao wafuga,
👉Ni vema kuwahi kuweka viota bandani ili kuku wazoee kuingia na kutoka kwenye viota hivo walianza kutaga hawataanza kutaga wengi chini, *Ukichekewesha Viota utakutana na changamoto kubwa ya Kuku kutaga nje ya Viota*
*TATU: KUINGIZA KUKU KWENYE CAGES*
👉Kutokana na Aina ya kuku unayoifuga, ni vema kufahamu muda sahihi wa kuingiza kuku kwenye Cage,
👉Zipo cage za kulelea *vifaranga* 👉Zipo cage za Kuku *wakubwa* Nivema kuhamisha ndani ya Muda unaoshauriwa.
👉Kwa kuku wa Mayai inashuriwa wanapo kua na Umri WA *wiki 12-15* wahamishiwe kwenye cages kuzoea mazingira tayari Kwa kuanza kujiandaa kutaga , Usiwacheleweshe ili *Wasipate stress ya mazingira Pindi wanapo Anza kutaga mayai*
*NNE:MUDA WA KUTOA MARANDA BANDANI*
☝️Kwajili ya kuzingatia afya ya kuku wako ni vema Banda kuwa na hewa Safi, Randa kavu zisizo na vumbi jingi,
👉 *BROILER* , Inashuriwa Randa kubadilishwa baada ya *Wiki 2* ,itegemee jinsi zitakavokua zimeloana, Ila wafugaji wengine hawabadilishi Randa, Wanatoa Randa mbichi na kuweka Randa kavu , zisizo *Baada ya Kuvuna kuku Ndipo Hubadili Randa na kusafisha Banda kuweka mpya tayali Kwa Batch nyingine*
👉KUKU WA *MAYAI* , *CHOTARA* , *ASILI*
👉Iwapo Banda lako limejengwa katika ubora STAHIKI ( *kuruhusu hewa kuingia na kutoka ipasavyo).* Unaweza kufuga kuku Batch nzima bila kubadilisha Randa, ( *Unatoa zinazoloa na kuzigeuza geuza Kwa rake)* .
👉Mabanda yasiyo ruhusu Sana hewa kupita , inashauriwa Randa kubadilishwa walau Kwa miezi mitatu *mara 1 au 2*
☝️ Ukizingatia utapunguza Sana magonjwa magonjwa ya Mfumo wa hewa mfn *Mafua* na Kuhara Damu( *Coccidiosis* ).
*TANO: UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU*
☝️Ni vema kutunza kumbukumbu za mradi wako Kwa kila gharama unayo itumia
👉Chakula
👉Tiba na chanjo ( *Dafatari lioneshe dawa zikizotumika Kwa Mpangilio na chanjo* ).
👉Vitamins
👉Daktari
👉Vijana
👉Mauzo ( Kuku, Vifaranga, mayai, Mbolea).
👉N.k Vyote vionekane kwenye kumbukumbu mashambani
☝️Hii husaidia Kufanya tathmini ya maendeleo ya mradi au kama unapata faida au hasara( *KITABU CHA KUMBUKUMBU PDF NI 3000 )*
*SITA* : Ainisha changamoto kuu za shamba lako ili kila mara UWE unapambana kuzipunguza Kwa mradi endelevu.
*TUISHIE HAPA KWA LEO*
👉 *Kitabu Chenye masomo yote kutoka Kwangu PDF SASA kinapatikana Kwa 5000 Tu.*
☝️Share bila Kuondoa utambulisho WA Mwandishi☝️
WhatsApp 0769799728 nicheki

0 Comments