*JINSI YA KUTENGENEZA SEHEMU YA KULELEA VIFARANGA/ BROODER:*
*BROODER* kwa jina lingine unaweza kuita ( *kinengunengu*), hii ni sehemu ya muhimu sana , na yakuzingatia sana wakati wa *MALEZI ya *VIFARANGA*
*SIFA ZA BROODER BORA*
👉Joto lakutosha
👉Randa/matandazo
👉Maji
👉Chakula
👉Hewa ya kutosha
👉Mwanga
👉Nafasi ya sahihi ya kutosha
*🐤NINI SASA UNTAKIWA KUFANYA KUANDAA BROODER/ SEHEMU YA KULELEA VIFARANGA.*
👉Kwanza angalia idadi ya vifaranga wako,
👈Brooder inaweza kuwa ya duara, kama utalea vifaranga wachache
👈Kama utalea vifaranga wengi unaweza kutengeneza brooder ya pembe nne kwa kuzingatia vipimo.
*MATENGENEZO YA BROODER YA DUARA*
👉Tafuta siling board, ikate kwa urefu vipande vitatu (standard 30-40 cm) kimo, au wengine hukata Mara mbili *(katikati)*
👉Unganisha vipande ulivyo vikata kutengeneza duara lako, Mimi huunganisha kwa kuchana kibao kwa msumeno kitakacho shikilia siling board upande wa juu kwenye maungio.
👉Kitaalamu mita moja mraba hutosha vifaranga 40, ila eneo utakua unalitanua kwa kadri vifaranga watakavo kua wanaongezeka kukua.
👉Baada ya kutengeneza brooder yako, Weka randa za mbao au pumba ya mpunga ( walau wiki 1 kabla ya kuleta vifaranga)
👉Tandika gazeti, au mifuko, au Ground paper.
👉Wakati vifaranga wanakaribia masaa kadhaa kabla vifaranga kufika weka chanzo cha joto ( vyungu, Bulb, Gas heater). Kama chumba nikikubwa sana na joto litachelewa kushika kwenye sakafu washa masaa 24 kabla ya vifaranga kufika, Joto la sakafu, randa , na maji vinatakiwa vifikie joto la chumba.
👉Ingiza vifaranga wako, tayari wakute chakula na maji bandani,
👉Hakikisha vifaranga wanapata chakula na maji muda wote ili wakue kwa uwiano, hasa wiki 2 za kwanza , ukikosea tu watapishana ukuaji
👉Vifaranga waanze kwa chakula cha Starter kwa wiki 6-8 za kwanza kwa kutegemea maelekezo ya chakula unacho tumia.
*WENYE VIFARANGA WENGI*
👉Andaa chumba chakulelea vifaranga ,kama kawaida
👉Weka joto, vyombo vya maji, vyombo vya chakula
👉Hakikisha sana kama unatumia, mkaa madirisha yako yanakua yanaruhusu hewa kuingia , unaacha uwazi kidogo kuepusha baridi kuingia bandani
👉Vyanzo vya joto viwepo bandani walau Massa 24 kabla ya vifaranga kufika kuleta joto kwenye sakafu na randa
👉Tandika magazeti, au mifuko kwa siku 3-5 na ubadilishe kila yatakapo chafuka ( *kila siku*)
👉Chakula na maji viwekwe masaa mawili kabla ya vifaranga kufika
👉Mita moja mraba vifaranga 40, eneo liongezeke kadri vifaranga watakao kua wanaongezeka
👉 *#KUMBUKA*: muda wa kufanya brooding unatofautiana, maeneo ya baridi wiki 3-4, maeneo ya joto wiki 1-2.
*VIASHIRIA VYA HALI YA HEWA BANDANI*
*👉BARIDI IKIZIDI* vifaranga wanakusanyika pamoja, au karibu na chanzo cha joto, suluhu ongeza joto
*👉JOTO LIKIZIDI,* viafaranga wanahema sana kwa kutanua mdomo, wanakaa pembezoni mwa brooder, wanaacha kula, wanakimbia vyanzo vya joto. Suluhu punguza chanzo cha joto
👉 Upepo mwingi vifaranga wanazunguka kwa makundi bandani, watakimbia eneo upepo unakoelekea kuja eneo upepo unapo ingilia, Kumbuka upepo unaoingia unakua na baridi
👉 Joto sahihi, Vifaranga hutawanyika vizuri bandani, na hula na kunywa maji, hivo ukuaji wao huwa wa kuwiana vizuri
By KAHISE

0 Comments