*MWONGOZO WA KUKU CHOTARA*
Imeandaliwa na
*Greyson Kahise*
Mtaalamu wa kuku
0769799728
0715894582
👉Nimuda sasa sijaandika mwongozo kuhusu Ufugaji wa kuku Chotara ( *Dual purpose birds).*
👆👉Kwanza KUKU CHOTARA NI KUKU GANI??? Hawa ni kuku ambao Wana asili ya ukienyeji, Ila wameboreshwa vinasaba vyao na kuongezewa uwezo wa *kutaga mayai na kukua haraka*
👉Kundi la Kuku Chotara Lina *Breed au Mbegu* tofauti tofauti *zinazotofautiana* kitabia na pia huwa zina *mfanano* Kwa baadhi ya Tabia zao
👆👉Kwa Tanzania tunao kuku Chotara WA Aina Mbegu nyingi kama vile
👆TANBRO
👆SASSO
👆KULOIRER
👆ISRAEL
👆MALAWI n.k
👉Kuku hawa niwazalishaji wazuri Ila hutofautiana Kwa idadi ya mayai, au uwezo wa kujaza nyama mapema.
*SIFA ZA KUKU CHOTARA*
👆👉Wanataga mayai mengi kuliko kuku wa asili ( kienyeji).
👆👉Wanauwezo wa kuongeza uzito haraka
👆👉Hawaatamii ( Huigiza kuatamia Kwa muda mfupi).
👆👉Huwa na Jogoo na tetea
👆👉Wanawezwa kufugwa kienyeji ( Ukuaji wao hautakua wa haraka kama ukiwafuga nusu huria).
👆👉Mayai Yao hayawi meupe Sana kama ya kuku wa asili.
👆👉Maumbo Yao ni makubwa
👆👉Huanza kutaga wiki ya 18-22
👆👉Wastahimilivu wa magonjwa kwenye mazingira sahihi.
👏 *NAMNA ZA KUWAFUGA*
👉Kwakua ni chotara , wanaweza kufugwa kwajili ya mayai na kwajili ya nyama
*JINSI YA KUFUGA KWAJILI YA NYAMA*
👉Kuku hawa wanaweza kufikisha uzito wa kuanzia kilo 1.8 -2 ndani ya wiki 9 ( TANBRO, SASSO).
👉Kwajili ya nyama ndani ya Muda wa wiki Tisa wanatakiwa kulishwa chakula cha Kuku wa nyama ( *Broiler* ) iwapo hutawalisha basi utalazimika kuuza wakifika miezi *mitatu Hadi mitano.*
👉👆Wiki mbili za Kwanza Broiler starter crumble.
👉👆Siku ya 15- 22 Broiler grower pellet
👉👆Siku ya 23-63 nakuendelea Broiler Finisher Pellet ( *Utapata kuku wakubwa na wenye Afya Sana).*
👆👉BEI za kuuza hutofautiana ndani ya wiki Tisa sokoni NI Kati ya *_10000-15000_*
👏 *KUWAFUGA KWAJILI YA MAYAI*
👉👆Broiler Starter siku ya 1-13
👉👆Layers starter wiki ya 3-8
👉👆Layer Grower wiki ya 9-18-21 ,watakapo Anza kutaga
👉👆Layers mash wiki ya 21 mpaka kutoa ( *watakapo Anza kutaga hasa wakifika asilimia Tatu)*
👉👆Chotara wanatofautiana viwango vya utagaji na wanao uwezo wa kutaga mayai *180-240 au zaidi* Matunzo sahihi yanahitajika.
*CHANJO*
👉👆Kama ilivo Kwa Aina nyingine za Mifugo chanjo NI kitu cha muhimu Sana kukizingatia ili kuepusha hasara zisizo za Lazima.
👆👉Mifumo ya chanjo imwtofautiana kutokana na Maeneo unapo wachukua kuku ( *Ni vema ukaulizia kupewa Ratiba sahihi Kwa Aina ya kuku unao wanunua).*
INAYOTUMIKA SANA ILI ISISUMBUE
👆 Siku ya 7 Newcastle /Kideri
👆Siku ya 14 Gumboro/IBD
👆Siku ya 21 Newcastle/Kideri
👆Siku ya 28 Gumboro
👆Wiki ya 4-5 ( siku 30-35 Ndui )
👆Kila baada ya miezi 2-3 Newcstle
👉 *Wape Dawa ya minyoo* wakifika miezi miwili , kisha kila baada ya miezi 3
*NB* : RATIBA ZA CHANJO ZINAWEZA KUTOFAUTIANA KUTOKA SEHEMU MOJA KWENDA NYINGINE ( Ndui Kwa sasa maeneo mengine inachanjwa mapema Kati ya Siku *21-25* ).
👏🐓👆👉 *ZINGATIA*
👉Chakula Bora na Ratiba sahihi na kipimo cha chakula ( ukikosea wanadumaa au hawatagi Kwa wakati)
👉👆VITAMINS ( *Bila KUKOSA kuepusha shida ya macho)*
👉Usafi wa maji na chakula
👉Banda Safi na salama dhidi ya vimelea
👉Hakikisha umetafuta masoko
👉Usitumie dawa bila ushauri WA Dr au mtaalamu ( *Dawa sio chakula)*
👉Zingatia Chanjo
👉Weka kumbukumbu zote Ipasavyo
👉Jali wafanyakazi wako
👉 *Kumbuka Kula bidhaa za Kuku na familia na watenda kazi*
Imeandaliwa na
*Greyson Kahise*
Mtaalamu wa kuku

0 Comments