NIONGELEE KUHUSU UKUBWA WA MAYAI

IMEANDALIWA NA

 GREYSON KAHISE 

 MTAAALMU WA KUKU

 0769799728 0715894582



Kwa uzoefu wangu kuku huwa wanaanza kutaga Kati ya wiki ya 17-20 Kwa breed nyingi iwapo utawakuza wanavo yakiwa kukuzwa

🔥Kuku wakianza kutaga hawaanzi wote hivo huchukua wiki 5-6 ili kuku wengi bandani wawe wameanza kutaga Mfnwakianza wikiya 18 tunatarajia wiki ya 24-26 kuku wawe wamechanganya kutaga

👏Katika umri huu ambapo mayai yatakua yanaongezeka Kuku , Yapo mayai ambayo yatakua makubwa na yapo mayai ambayo yatakua madogo

Ila wakishataga Kwa wastani WA miezi miwili huwa tunategemea kuku wawe na mayai ya size moja ( Makubwa yanayo kubalika sokoni)

👉Kama alivo sema mwanagroup mmoja Breed kama Hyline ( HUANZA kutaga wakiwa na umbo dogo hivo mayai HUANZA na size ndogo kiasi Ila baada ya miezi miwili mayai Yao huongezeka umbo na kuwa lenye kufaa sokoni).

👉Bovans brown na ISA brown wenyewe HUANZA na mayai makubwa kiasi kutokana na maumbo Yao PINDI wanapo Anza kutaga Ila Bovans wanaanza Sana Ku wiki ya 20 wiki mbili baada ya Hyline kuanza kutaga

👏 BAADHI YA MAMBO YANAYOWEZA KUFANYA UMBO LA YAI KUWA DOGO KWA MUDA MREFU

👉Poor uniformity ( Uwiano wa ukubwa wa kuku, kiumbo na uzito) Iwapokukuwako wataanza kutaga wengine wakiwa na 1.7 kg na wengine 1.3 kg hii inaashiria kwamba mayai Yao yatachukua muda mrefu kuja kuwiana size bandani ( hivo ni vema kuwapima kuku mara Kwa mara kujua maendeleo Yao ili ufanyejeee maamuzi mapema kama uongeze chakula au laa).

👨‍🦯Kitaalamu kuku anaekuwa ( growers ) hawapaswi kupunguziwa  chakula Ila unaweza kusimamisha kuongeza chakula iwapo uzito wao utakua mkubwa kupindukia ( chakula kinaweza kupunguziwa Tu baada ya kuku kuwa wametaga Kwa muda mrefu ishauriwe na Farm manager au DAKTARI)

👉Magonjwa ( Ni ukweli usiopingika kwamba matumizi makubwa ya dawa zenye salfa kipindi cha ukuaji huathiri Kwa Sehemu maendeleo ya utengenezaji wa Mfumo wa yai ndio maana ukichukua Ufanisi WA utagaji Kwa kuku alietumia dawa Sana na alietumia kiasi itakua tofauti kabisa) Kuku waliotumia kiwango kikubwa cha dawa NI nadra KUFIKISHA 90% ya utagaji na hawawezi kutaga Kwa kipindi kirefu ( Percistance itakua ndogo)

👏MWANGA hili tutalipa kipindi kimoja tufundishe umuhimu wa Mwanga tangu akiwa kifaranga, Akiwa kwenye Growers stage na Akiwa kwenye Production ( Mwanga Una mchango mkubwa Sana kwenye idadi ya mayai na size ya mayai tutafundisha Kwa upana).

🔨 CHAKUL Moja ya sababu kubwa zinazopelekea utofauti mkubwa Iwapo chakula hakita kuwa na Energy ya kutosha basi kuku wengi hawatataga na size pia itaathiriwa ndio mana kama kuku again kutaga mayai kwa kusua SUA huwa tunashauri Punguza pumba ongeza mahindi 

🔨Chakula Bora sio Tu NI mwarobaini Ila Mfumo wa ulishaji pia unapaswa izingatiwe sana ( Mfn MIMI NAWEZA TUMIA COMMERCIAL LAYERS KAMPUNI X NA WEWE UKATUMIA HIYO HIYO KAMPUNI X Ila Mimi nikapata matokeo wewe ukafeli KWANINI ⁉️

👉Muda wa kulisha usibadilike kila siku uwe uleule 

👉Pima kiwango sahihi kutokana na umri na idadi ya kuku

👉Vyombo vya chakula vitosheleze idadi ya kuku bandani Kwa uwiano sahihi.

🙌 MAJI  Kuku anakunywa maji mara 2-2.6 ya chakula anacho Kula ,ukiona kuku wamepunguza kunywa maji Leo usitegemee kupata mayai mengi Kesho ( pambana kujua sababu ya kupunguza unywaji WA maji na Maji yawe masafi na yawepo muda wote).

PINDI TUKIONA PAMOJA NA SABABU NYINGINE ZOTE  kuku hawatagi mayai makubwa tunashauri matumizi ya GLP kusaidia kuboost size ya mayai

Nimeandika Kwa muhtasari Kwa baadhi ya vitu vya msingi kuzingatia Kwa kuku wa mayai 

 MFUGAJI WA LAYERS WAWEZA NICHEKI KWA NAMBA HIZO TUSHAURIANE ZAIDI

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓