LEO NATOA FUNZO NJE YA UFUGAJI WA KUKU ILA UNAWEZA KUHUSIANISHA NA UFUGAJI WA KUKU
IMEANDALIWA NA
Greyson Kahise
Mtaalamu wa kuku
0769799728
0715894582
Natambua Sana kwamba ndoto au kiu ya kila mjasiliamali huwa ni Kufikia mafanikio ambayo anahatamani Kwa kufananisha na mtaji, juhudi, maarifa n.k
Naomba nifundishe somo hili Kwa mifano halisi Tu kutoka kwangu Mwenyewe.
Moja : HARDWORK/BIDII
👉Moja ya kitu ambacho bado naendelea kujifunza na kuona kina manufaa makubwa yasiyo fichika ni Kufanya kazi Kwa bidii.
👆Hii nimeithibitisha Mwenyewe binafsi hasa pale nilipo jiambia natamani niwahudumie wafugaji kuongeza UJUZI na kuongeza uzalishaji kwenye miradi Yao ya kuku,
👆Nilijituma Sana kuandika masomo, kuwakutanisha wafugaji pamoja na mengine mengi pasipo kukata tamaa na nimeanza kuona mafanikio kwenye lengo langu la swali.
Mbili: SACRIFICE/KUJITOLEA
👆Sio kila unachokifanya nilazima kiwe kinakuingizia pesa, wakati mwingine unapaswa Kufanya kama huduma ili kumuwezesha mwingine pasipo kujali utanufaika vipi Kwa muda huo.
👉Hii imenisaidia nimekua si mtu wa kukata tamaa kutoa huduma hata kama sikila ninachofanya kinanilipa , Ila najivunia huduma kwajili ya wale ambao wamerudi kwangu na kutoa shuhuda za KUFANIKIWA na kunipa SHUKURANI zao kunifanya nifurahie huduma yangu kwao.
Tatu: STRUGGLE/ KUPAMBANA ( KUFIGHT).
👆Hakuna mafanikio rahisi, Kwa mana hiyo hainabudi kukomaa kupambania unacho kiamini, Mimi binafsi nimekua napambania ndoto yangu kila siku tena bila Kuchoka , naona mwelekeo japo sio kazi ndogo vikwazo vipo vingi Sana njiani
👆Nilipata wazo la kuandika kitabu cha Ufugaji kuku nikafanikiwa kuprint , nikafanikiwa kuuza nakala kadhaa, haikua rahisi Ila nilipambama bila Kuchoka ili kuitimiza kiu yangu na nikafanikiwa na sijaacha kupambana kulifanikisha zaidi.
Nne: FAITH /IMANI
👆Kama huta kuwa na Imani na Kile unacho kiamini, mafanikio itakua ni ndoto ya abunuasi, kwasababu hautakua na moyo wa dhati wa kukipambania unacho kutafuta
🔥Mimi nilijiaminisha kwamba nikisimama Imara Kwa kutoa huduma sahihi Kwa wafugaji, nitawawezesha kusonga mbele kidogo, na kupitia wao nitakutana na marafiki wapya na wataniwezesha kupiga hatua kimaendeleo, YES Imani yangu inazidi kunipa picha na kufanikiwa siku Kwa siku na Bado naamini ITATHIBITIKA
Tano/ PATIENCE/ UVUMILIVU
👆Kwenye mradi wowote, ukikosekana UVUMILIVU Tu ni ngumu Sana Kufikia Malengo, hii ni dhahiri hata kwenye Ufugaji wa kuku, kuwekeza pesa sio uhakika kwamba ni lazima pesa hizo zikuletee faida, kuna muda ni lazima ukubali kupoteza ili kujifunza, kupoteza ili uimarike, kupoteza ili usahihishe makosa, na Kadri unavyo zidi kupunguza makosa ndipo utaanza kuona Mwanga WA mafanikio taratibu taratibu
👉Nilifuga kuku wangu Kwa mara ya kwanza walikufa zaidi ya 120, sikukata tamaa, nilizalisha vitabu Kwa mara ya Kwanza ilinichukua muda mrefu Sana kuuza, Ila haikua sehemu ya Mimi kuacha kuwa mvumilivu MSEMO WA MVUMILIVU HULA MBIVU NI KWELI
Ukijumuisha hayo mambo , hapo juu amini kwamba utafanikiwa hatua Kwa hatua, utapitia changamoto nyingi, fitna nyingi, vikwazo vingi, na magumu mengi, Kwa kadri unavo zidi kupambana bila kukata tamaa , Amini kwamba UTAFANIKIWA KABISA.
ASANTE KWA KUSOMA KAMA USIPO ELEWA NIPIGIE SIMU NIKUELEWESHE.


0 Comments