SOMO KUHUSU VIFARANGA



Hii Imeandaliwa na:

GREYSON KAHISE

MTAALAMU WA KUKU

 0769799728

 0715894582

Kwa Kifupi Sana fanya yafuatayo utanishukuru

Kwanza kabisa vifaranga wanahitaji Sana Mambo yafuatayo yazingatiwe.

👉Joto

👉Chakula Safi

👉Maji Safi

👉Mzunguko mzuri wa hewa

👉Idadi sahihi ya Vyombo vya chakula na Maji

👉Randa Safi ,zisizo na vumbi, kavu

👉 Biosecurity/ usalama wa viumbe.

NISEME TU KWAMBA FUATA HAYA KWA VITENDO KABISA UTAFAULU

👉 WIKI LA KWANZA

👆Siku ya kwanza kabisa ( Glucose/Glucovet.. inategemea wametoka umbali gani wanaweza kupewa masaa 3-24).

👆 Multivitamins Mfn! Neoxychick, Chick formula ,Tetracovit Kwa siku ya kwanza Hadi ya 5 ( SIJAANDIKA DAWA HAPO).

👆Siku ya 6 huwa tunashauri wapewe maji tupu, 

👆Siku ya Saba ni chanjo ya kwanza ya NEWCASTLE/ KIDERI-MDONDO

👉Muda huu wote watakua wanatumia chakula cha Starter/ Broiler starter.

WIKI LA PILI

👆Siku ya nane Hadi siku ya 12  Wapewe vitamins zipo Aina nyingi Sana Mfn :Aminototo, Farmvita, Dad OCTAVIT, Amylyte, Vitalyte n.k

👆Siku ya 13 wapewe maji matupu ( japo hata ukiwawekea vitamins si mbaya).

👆Siku ya 14 wapewe chanjo ya Pili ya Infections Bursal Disease / Gumboro

👉 Muda huu wote wapewe chakula cha Starter/ Broiler Starter.

WIKI LA TATU

👉Hapa tuna wagawa kuku kutokana na Aina

👆 KUKU WA NYAMA/BROILERS

👉Siku ya 14  au15 Hadi ya 22 wapewe Grower Pellets ( Kwa uzoefu wangu). 

👆Hapa hawa kuku wanaweza kupewa Broiler Booster Mfn : Utravin broiler booster.

👆Siku ya 21 kuku Broiler wapewe chanjo moja wapo Kati ya Gumboro au KIDERI  ( Hii inategemea MAZOEA ya namna ya kuchanja kuku kutokana na mkoa ulipo). 

👉 KWA KUKU  WANAOANDALIWAKUTAGA ( CHOTARA, LAYERS , KUKU WA KIENYEJI).

👆Wapewe chakula cha Starter Mashi inaenda mpaka wiki ya 7 au wiki ya 8 (inategemea maelezo ya chakula unachotumia na kampuni uliyo nunua chakula).

👉Siku ya 21 kuku hawa watapewa Chanjo ya pili ya Newcastle/KIDERI/MDONDO

👆Siku ya 28 kuku wanao andaliwa kutaga wapewe chanjo ya pili ya Gumboro

👆Siku ya 30-35 ni chanjo ya Ndui (Japo maeneo mengine Ndui hutokea mapema wiki ya 3).

👉Kila baada ya miezi mitatu  kukuwako wapewe chanjo ya KIDERI/ Newcastle

KUMBUKA

👉 Minyoo ni hatari Sana Kwa maendeleo ya kuku....unapaswa kuwapa dawa za minyoo mapema Kwa mara ya kwanza wakifika miezi miwili , 👉Kisha utakua unarudia kila baada ya miezi mitatu USIPUUZE

👆Kwa chakula wape grower mash wiki ya nane au 9 mpaka wiki ya 18-19 ( Pale utakapo okota yai bandani).

NB : Kuku hawa wapewe vitamins mara Kwa mara ..sio lazima kuwapa kilasiku kupunguza Gharama

👆Kuku wako wakifikisha asilimia 3-5 za utagaji wape Layers mash moja Kwa moja Hadi pale utakapo amua kuja kuwauza

Ikumbukwe kuku hawa wanapaswa Kula Kwa kipimo maalumu kutokana na Umri

👆 MAZOEA YANAONESHA WATU KUFUGA KWA KUWEKA RATIBA YA DAWA KAMA CHAKULA

👉 Hii sisawa Kitaalamu , kuku wapewe dawa pindi wanapoumwa...Uzoefu wangu haunioneshi ulazima WA kukuza kuku Kwa Dawa.

Asante na karibu sana