TUKUMBUSHANE KIDOGO

 Imeandaliwa na 

Greyson Kahise

Mtaalamu wa kuku

0769799728

 0715894582



Kama ilivo Kwa viumbe wengine, Chakula Bora, Afya njema, Utimamu wa Mwili ni njia Pekee, ya kuboresha au KUONGEZA uzalishaji Kwa MIFUGO hiyo,

Mfn : Wakati Ng'ombe au Mbuzi anakamuliwa , huwa tunaweka chakula ale ili awe Sawa na kutusaidia kutoa maziwa,  kama hutampa chakula muda huo atapunguza kiasi cha maziwa siku husika

👏Hii haina utofauti Kwa mfugo KUKU, kuku ni kiumbe Ndege nae anahitaji matunzo Yale Yale Kwa KUTEGEMEA miongozo yake ili HATIMAE , AMA auzwe ndani ya Muda Kwa nyama, au ATAGE mapema mayai mengi na yenye size yakueleweka

👆🏿Moja ya malalamiko ambayo nimekua nikipokea mara Kwa mara kutoka Kwa wafugaji ni Kuku kuvimba macho na kujaa kama tongotongo ndani au kutoa machozi

👆🏿Ila ukiuliza Sana wafugaji Ratiba zao za kuwapa kuku vitamins zinatia mashaka, Mfn Mfugaji atawapa kuku wake vitamins hasa wiki tatu za Mwanzo na kuacha Hadi inapotokea tatizo ndo anakuja kuanza kuwapa tena , hii inakua si Sawa na unakua umechelewa sana.

🐓Nishauri Tu kwamba , vitamins Kwa kuku NI muhimu Sana, binafsi KAHISE Kwa uzoefu wangu nashauri kuku wapewe vitamins *lMfululizo Tu bila Kuchoka wakiwa kwenye Brooding ( Mwezi mmoja wa Kwanza)

👆🏿Kisha baada ya huo umri wa Mwezi mmoja , wa Mwanzo unaweza jiwekea utaratibu wa Kuwapa kuku Vitamin kila baada ya siku 10 unawapa vitamins Mfululizo Kwa siku 5 Hii itakusaidia Sana kupunguza changamoto za magonjwa ya nayosababishwa na upungufu WA vitamins Mfano AVITAMINOSIS, au Encephalomalacia ( Crazy chicks, kuku kuzungusha shingo kna kwamba ana mdondo).

Tukifanya hivo itatusaidia Sana kupunguza vifo vinavyo epukika.

 NB

👆🏿 :Usafi wa Banda muhimu Sana

👆🏿Usafi wa vyombo vya maji na chakula muhimu Sana

👆🏿Kuzingatia Ratiba za chanjo, dawa za minyoo na muda wa kulisha kuku muhimu Sana.

👆🏿Kulisha kuku kiwango sahihi na masaa ya Mwanga muhimu Sana.

👆🏿Kutunza kumbukumbu Muhimu Sana

👆🏿Kutumia wataalamu kwenye mradi endelevu wa kuku Muhimu Sana

👆🏿 KULA NA KUENJOY MAISHA KWA BIDHAA ZA KUKU NDIO FAHARI YETU

 FANYA KAZI KWA BIDII ILA USISAHAU KULA NA KUISHI VIZURI

Nitafute Kwa huduma zifuatazo

👆🏿USIMAMIZI WA MRADI WA KUKU

👆🏿 VIFARANGA

👆🏿USHAURI KUHUSU KUKU

👆🏿VITABU BORA VYA UFUGAJI WAKUKU

👆🏿FORMULA ZA CHAKULA CHA KUKU

 KARIBUNI SANA I LOVE CHICKENS