*Greyson Kahise*
Mtaalamu wa kuku
0769799729 0715894582
*MOSHI KILIMANJARO*
*Hellow habarini*
*SWALI* : Naomba kama kuna mtu wa uchumi humu , atuandalie somo linalo husianisha Ufugaji wa kuku na uinuaji wa kipato kwa mfugaji
👆👉Wafugaji wengi wanafuga ila wanakosa mitazamo ya kiuchumi kubadilisha mradi kuwa pesa.
Part A by NASHON ELIA
*(Mwanauchumi)* +255 752 173 419
👉Somo linalo husianisha ufugaji wa kuku na kuinua kipato kwa mfugaji ili likamilike ni kitabu cha kurasa 200.
*@Hapa nitatoa vidokezo vichache tu;*
*1) LENGO/KUSUDI*
Akili ndiyo inayo design kila kitu kinachukuwa kwenye maisha yako. Kile utakachokusudia kufanya ndicho kitakacho tokea. Asiyejua aendako hapotei; hii inamaanisha kwamba kama utafuga bila malengo, chochote kitakachotokea kwenye mradi wako ndicho mafanikio yenyewe. Hata ukitokea ugonjwa ukaua kuku wote itakuwa ni hali ya kawaida tu. Kumbe ramani ya ufugaji ni malengo yako. Malengo makubwa hubeba mafanikio makubwa.
*2) MTAZAMO*
Unautazama vipi mradi wa ufugaji uliokusudia kufanya? Kila biashara unayoijua ni ndogo na pia ni kubwa. Ukiwa na mtazamo mzuri juu ha mradi wa ufugaji wa kuku utatarajia utajiri mkubwa, ukiwa na mtazamo hasi utatarajia kumchinjia shangazi yako siku atakapo kutembelea umpe mapaja yote mawilk ale akushukuru. Unapotia mguu kwenye ufugaji wa kuku fuga kweli usifanye jaribio la ufugaji. Kwasababu ya ushindani wa soko faida ya mazao ya kuku huwa ndogo. Ili faida hiyo iinue uchumi wako unatakiwa kuikusanya kwa wingi. Yani kama banda moja linaweza kutoa faida ya 20,000 kwa siku basi lenga kuwa na mabanda 30 ili upate 600,000 kwa siku. Kadri unavyowekeza zaidi ndivyo utakavyopata zaidi. Epuka mitazamo dhaifu. Epuka kusema siwezi. Jenga mtazamo wa mafanikio utafute mafanikio siyo kutafuta sababu za kushindwa.
*3)HOFU*
Epuka kuogopa hasara. Uchungu wa nyanyachungu ndio utamu wenyewe. Kuku kuugua hata kufa ndio ufugaji wenyewe. Wakifa ni faida maana utajifunza na kuelewa kwanini wamekufa hivyo mara nyingine utaweza kudhibiti wasife. Usiogope ushindani wa soko maana hata leo wateja wapya wa mazao ya kuku wamezaliwa. Kuwa jasiri usiogope changamoto yoyote.
*4) IMANI*
Yote unayofikiria yapo ila kile unachoamini ndicho kitakachotokea.
*5) SHAUKU*
Usiyaonee wivu mafanikio ya yule muhindi kwenye ufugaji pale Arusha bali uwe na shauku ya kufuga ufikie kiwango chake. Ukiona wafugaji wakubwa wanatawara soko vibaya usikimbie. Jenga shauku ya kuwapita uwe mkubwa zaidi yao.
*Part B*
By Neema +255 762 582 423 *(mwanauchumi)*
👉Kuna kitu kinatwa SWOT analysis.
Kirefu chake *(strength* *weakness* *opportunity* and *threat* .
👉Kitambue kitu unacho wrza kukifanya kwa usahihi kabla ya kuamua kuanza kukifanya( *pata elimu* )
👉Jijue uwezo wako kwenye ufugaji aina gani ya kuku unaweza kufuga ; uwezo wa kiuchumi kuweza kugharamia aina ya kuku unaotaka na Muda ulionao hiyo ni *strength.*
👉Wapi huwez kufanya vizur ili uweze kurekebisha hii ni *weakness* tambua udhaifu wako upo hasa sehemu ipi upatilie mkazo zaidi. Mfn kama ni magonjwa, utafute elimu zaidi, au utafute *Daktari unae mwamini zaidi.*
👉 *Opportunity/Unaona* fursa gani ukiamua kufuga ambapo litakua labda soko la dhaa au manufaa kulingana na mahitaji yako.
👉 *Mwisho threat* . Ie Who are ua competetors/ watambue washindani wako kibiashara; ukiwatambua tafuta mbinu ya kwako ya kuwapiku Ili nawewe uingie kwenye mnyororo wa soko
*Mfn: Pata namna bora za kukuza kuku kwa kiwango kidogo cha madawa* , matumizi ya vyakula visivyo tumia gharama kubwa kupatikana n.k
*Tambua hii ni kiu yangu ya dhati kuona mfugaji unajikwamua kupitia juhudi zako, Masomo haya yatumie kwa kutafsiri mradi wa aina yoyote unao tarajia kuufanya utafanikiwa.*
🤝 *Part C* ; Mwanauchumi Neema.🤝
*Mwongozo kutoka kwa mmoja wa wanauchumi* .👇👇👇
👉Habari wafugaji mimi nitaeleza kwa ufupi Sana hatua za kufanikiwa kiuchumi ukizifuata zitakukomboa, ila kitu Cha kwanza jijue wewe Ni mtu sahihi wa kufanya unachofanya?
Jitathimini ujuzi wako ili kukusaidia kuamua iwapo unafaa kuanzisha biashara/mradi wa kuku,
Angalia Kama una mapungufu au uwezo(elimu), Kama una mapungufu ya elimu ya ufugaji wa kuku tafuta jinsi ya kuziba hata kwa asilimia ndogo; watu wengi tunakwepa gharama Sana jitoe kupata elimu ya ufugaji( semina, Nk, vitabu)
*👇Hatua za kufuata kufanikiwa kiuchumi Ni:*
1: *visibility/Maono*
Lazima ujue unataka nini,/uwe na picha kamili ya project/mradi wako otazamia kuanzisha hii itakusaidia Sana.
2: *Information* (maelezo/taarifa)
Ni lazima uwe na taarifa/maelezo sahihi ya mradi wako wa kuku unaoutaka, yaani ujuwe kuku utapata wapi, utakuzaje, masoko yapoje ,vyakula utapataje, madawa utapata wapi n.k
*NB:* Pata elimu ya kuhusu kuku, pia angalia mtu unayemuuliza ili kupata taarifa
👉Asiwe mtu mwenye mawazo finyu (aliyeshindwa)
👉asiwe mkatisha tamaa
👉Asiwe mwenye wivu
Unaweza pata maelezo ambayo sio sahihi ukajuta mbele
3: *Strategies* (mikakati)
Tenga muda wako na Mali ili uweze kufanikisha unachokusudia, pia usione tabu kutumia wataalamu unao waamini.
👉Kama mradi nu mkubwa pia unaweza ukaufanikisha kwa hatua moja baada ya nyingine ili ufanikishe kwa uzuri/ufanisi zaidi. *(Gawanya mradi kwa phase)*
4: *Implementation* (utendaji/utekelezaji)
Fanya kile ulichokuwa nacho yaani ile picha uliyonayo ya mradi mwanzoni na kuamua kile ulichoweka kwenye mikakati yako usibadilike badilike
👊Amini unaweza
👊Fanya kwa bidii
👊Uvivu hautakiwi
👊Usile mtaji hata iweje
👊jitangaze biashara yako.
👉 *Kwa kifupi maelezo Niliyotaka kutoa hayo yatakusaidia ukiweka kwenye utekelezaji wa mradi wako*
Hii tumeitoa kwa kutazama mradi wa kuku, Ila unaweza kuitafsiri na kuiweka kwenye mradi mwingine wowote na utafanikiwa
Imeandaliwa na
Neema +255 755 273 235 ( *mwanauchumi)*
Kwa kushirikiana na
Greyson Kahise mtaalamu wa kuku
0715894582
0769799728

0 Comments