*MAELEZO KUHUSU ANTIBIOTIC.*

Imetolewa Kwenu na 

 *Greyson Kahise* 

Mtaalamu wa kuku

 *0769799728* 

 *0715894582*



SOMA ZAIDI KWENYE TOVUTI YETU

http://www.kukubiasharatz.com/2020/05/makala-juu-ya-mayaiya-kuku-na.html

Kwanza kabisa *Ant-biotics* kwa kingereza ni Against Living organisms ila kwenye matibabu hutumika kama against  *(Bacteria)* 

Ila lengo letu hapa sio kulitanua sana somo ila tufahamishane kuhusu matumizi ya *Antibiotic* .

 *Twende sawa sasa*

👆 *Antibiotics* ni tiba ambazo zimejikita sana katika *kutibu* na sio kinga kama wengine wanavozitumia.

👉Antibiotics hufanya kazi kwa namna mbili mwilini mwa kiumbe ikiwa ni- Kusitisha uzalianaji wa bacteria( *Bacteriastatics)* na kuua bacteria *(Bactericidal)* 

👏Kuna neno la kimatibabu kwa baadhi ya dawa kama OTC zimeandikwa *Treatment* and *Prophylaxis*

👉 Treatment ni tiba kwa ugonjwa ambao tayari umesha jitokeza.

👉Prophylaxis, hii inafanywa na dawa ikiaminika kwamba tayari huyu kuku ameshapata maambukizi hata kama bado ugonjwa haujajitokeza ( *kwa mana hiyo inapunguza uwezekano wa ugonjwa kujitokeza ila sio kuwa inakinga ugonjwa* ) Dawa ambazo zimekua zikitumiwa hasa kwa Prophylaxis ni Broad spectrum Antibiotic kama *OTC* tunawapa ndani ya muda flani( *incubation period* ) kwa hiyo basi

Pia Prophylaxis mnyama hupewa dawa yenye dozi ndogo sana kuliko pale utakapo kuwa unatibu( *inahitaji daktari abaini kwanza dalili za maambukizi ndipo ifanyike* ) 

 *Mfn:* Kuku akipata ndui huwa tunashauri apewe *OTC* ili kuzuia vimelea wengine kama bacteria wasiingie kupitia vidonda, Tunacho fanya ni kuzuia maambukizi ya pili/ Secondary bacterial infection kupitia vile vidonda vinavyokua vimejitokeza kwa kuku. Hii ni kwasababu kirusi cha ndui kinadhoofisha kinga ya mwili.

ANTBIOTIC sio *KINGA* ni *DAWA* za kutibu.

👉Mwingine akawa ameuliza kwamba mbona kwenye chakula huwa kuna dawa zinawekwa

👉Kinachofanyika kwenye chakula huwa zinawekwa protozoa static mfano  Coccidiostats ambazo huzuia uzalianaji hasa wa protozoans ambazo zinasababisha magonjwa kama *Coccidiosis*  ila haitumiki kama kinga inatumika kama *Prevention/Kuzuia uwezekano.* 

Soma zaidi 

http://www.kukubiasharatz.com/2020/05/mwongozo-wa-manunuzi-ya-kuku-na.html

👉Tatizo moja kubwa la Bacteria huwa na Tabia ya kutengeneza Usugu ( *Drug resistance* )

Mfn: Kama utakua unawapa kuku wako madawa Mara kwa Mara , utafika muda kuku hawatasikia kabisa dawa hii ni sawa na *KUNGUNI* unaweza tumia dawa hata 100 na asife.

Kama wataalamu tunashauri sana madawa yatolewe pale unapobaini hasa ugonjwa husika, sio kila utakapoona kuku amesinzia ni kuanza kuwanywesha madawa.

 *KITU NAWEZA KUSHAURI*

Wafugaji tujitahidi sana kufanya management nzuri kuepusha kuku wetu kupata magonjwa Mara kwa Mara 

👉Usafi

👉Biosecurity

👉Chakula na maji safi

👉Panya na ndege wasiingine sana bandani.

👉Randa ziwe kavu N.K itatusaidia sana kupunguza hii case.

 *Tunaamini maduka ya madawa ya mifugo na yanatusaidia sana*

👉Ila kumbuka wauzaji wa madawa hawafiki kwa kuku, wanasikiliza maelezo yako kisha wanakwambia dawa pasipo kumchunguza kuku ,nivema basi mfugaji kama unaweza kukutana na Daktari au kufika Clinic Kukuwako achunguzwe ndipo ukanunue dawa

Kwa uzoefu mfupi nilipokua nazunguka kwa wafugaji, Ndani ya siku 3 mfugaji anaweza kununua dawa tofauti 3 kutibu ugonjwa m1 na hii *si sawa* tiba kwa kutegemea na dozi matokeo yataanza kuonekana baada walau ya siku 3 sio siku 1 ,mnaongeza usugu pia mnaongeza gharama kubwa sana za kuhudumia kuku.

 *NB: Kuku atakae kuzwa kwa madawa muda wote hawi mtagaji mzuri.*

💪💪💪 *Mwisho kabisa Anza na dawa za leval ndogo ndipo ufuate dawa za leval kubwa* 💪💪💪

*Unaweza kujisomea masomo yangu sasa Kwa tovuti yangu rasmi*

http://www.kukubiasharatz.com/2021/08/kuku-wa-asili.html

 *KARIBU SANA*