*TUKUMBUSHANE KIDOGO*
*Imeandaliwa* na
Greyson Kahise
Mtaalamu wa kuku
0769799728
*0715894582*
Kama ilivo Kwa viumbe wengine, Chakula Bora, Afya njema, Utimamu wa Mwili ni njia Pekee, ya kuboresha au KUONGEZA uzalishaji Kwa MIFUGO hiyo,
*Mfn* : Wakati Ng'ombe au Mbuzi anakamuliwa , huwa tunaweka chakula ale ili awe Sawa na *kutusaidia kutoa maziwa, kama hutampa chakula muda huo atapunguza kiasi cha maziwa siku husika*
👏Hii haina utofauti Kwa mfugo *KUKU*, kuku ni kiumbe *Ndege* nae anahitaji matunzo Yale Yale Kwa KUTEGEMEA miongozo yake ili HATIMAE , AMA auzwe ndani ya Muda Kwa nyama, au *ATAGE* mapema mayai mengi na yenye size *yakueleweka*
👆🏿Moja ya malalamiko ambayo nimekua nikipokea mara Kwa mara kutoka Kwa wafugaji ni *Kuku kuvimba macho na kujaa kama tongotongo ndani au kutoa machozi*
👆🏿Ila ukiuliza Sana wafugaji Ratiba zao za kuwapa kuku vitamins zinatia *mashaka*, Mfn Mfugaji atawapa kuku wake vitamins hasa *wiki tatu* za Mwanzo na kuacha Hadi inapotokea *tatizo ndo anakuja kuanza kuwapa* tena , hii inakua si Sawa na unakua umechelewa sana.
🐓Nishauri Tu kwamba , vitamins Kwa kuku NI muhimu Sana, binafsi *KAHISE* Kwa uzoefu wangu nashauri kuku wapewe vitamins *Mfululizo* Tu bila Kuchoka wakiwa kwenye Brooding ( *Mwezi mmoja wa Kwanza)*
👆🏿Kisha baada ya huo umri wa Mwezi mmoja , wa Mwanzo unaweza jiwekea utaratibu wa Kuwapa kuku Vitamin kila baada ya siku 10 *unawapa vitamins Mfululizo Kwa siku 5* Hii itakusaidia Sana kupunguza changamoto za magonjwa ya nayosababishwa na upungufu WA vitamins Mfano *AVITAMINOSIS*, au Encephalomalacia ( *Crazy chicks, kuku kuzungusha shingo kna kwamba ana mdondo* ).
Tukifanya hivo itatusaidia Sana kupunguza vifo vinavyo epukika.
*NB*
👆🏿 :Usafi wa Banda muhimu Sana
👆🏿Usafi wa vyombo vya maji na chakula muhimu Sana
👆🏿Kuzingatia Ratiba za chanjo, dawa za minyoo na muda wa kulisha kuku muhimu Sana.
👆🏿Kulisha kuku kiwango sahihi na masaa ya Mwanga muhimu Sana.
👆🏿Kutunza kumbukumbu Muhimu Sana
👆🏿Kutumia wataalamu kwenye mradi endelevu wa kuku Muhimu Sana
👆🏿 *KULA NA KUENJOY MAISHA KWA BIDHAA ZA KUKU NDIO FAHARI YETU*
*FANYA KAZI KWA BIDII ILA USISAHAU KULA NA KUISHI VIZURI*
Nitafute Kwa huduma zifuatazo
👆🏿USIMAMIZI WA MRADI WA KUKU
👆🏿 VIFARANGA
👆🏿USHAURI KUHUSU KUKU
👆🏿VITABU BORA VYA UFUGAJI WAKUKU
👆🏿FORMULA ZA CHAKULA CHA KUKU
*KARIBUNI SANA I LOVE CHICKENS*


2 Comments
Great
ReplyDeleteThanks
Delete