*MASWALI NA MAJIBU ,* 
Imeandaliwa na 
 *Kahise* mtaalamu WA kuku na *Dr Vicent* 
07697997288
0715894482
 
Swali:*Dawa za Kusafishia Mabanda* 

1. Pharmguard
2. Virocid
3. Hi-7
4. TH-4
5. D-4 Vet
6. VB 001
7. V-RID
nk....

 *Tunashauri badilisha Dawa kila baada ya mizunguko mitatu (3)* Usitumie dawa Aina Moja mwaka mzima vimelea huzoea dawa hivo inaweza kupelekea kubaki shambani

 *Swali:Hivi kuna humuhimu wakuchemsha maji ya chanjo..kama ni ya bomba?*

Jibu: Maji ya Bomba (haswa ya DAWASA, nk...) huwekewa Chlorine kwa ajili ya kuuza vijidudu.

Chanjo zetu tunazowapa kuku kwa njia ya maji pia huwa ni *virusi hai*. Hivyo, maji yenye chlorine huweza kuua hawa virusi na kufanya chanjo kuwa 'imekufa'.

Kuzuia hilo, tunashauri maji ya chanjo 
1. Yachemshwe   AU
2. Weka maziwa yasiyo na mafuta (mf. Maziwa ya unga)
3. Tumia dawa maalumu za maji ya chanjo (mf: Immune granules, Effiboost, Vaccsure, Cevamune, Bioblue, nk...)

Wale wa maji ya kisima au mvua pia hampo Salama sana kwani maji ayo yanaweza pia kuwa na madini mazito (Heavy metals) ambazo pia huathiri wale 'Virusi' waliomo ndani ya chanjo.

 *Jambo la muhimu kufahamu* : Sio kwamba kila siku ugonjwa unakuwepo bandani. Kuna mtu anaweza kufuga kuku wake hata bila chanjo yoyote na wasipate haya magonjwa endapo hayajaja!

👉Issue ni kwamba hujui muda, siku wala saa ugonjwa utakapokuja. Ndio maana tunachanja kama tahadhari.

 *Swali: Ni Muda gani Banda linapaswa Kupumzishwa kabla ya kuweka kuku wengine???*
 *Jibu:* Hatushauri kuweka kuku umri tofauti ndani ya banda moja hata kama utakua umetenganisha kwa partition.

👆Hii inaleta changamoto kubwa kuzuia haya makundi yasiambukizane.

Kwa Wafugaji wa aina hii, kupumzisha banda kwao inakua changamoto maana Huwezi sema umepumzisha upande mmoja then upande mwingine una kuku.

👆Ukitaka kupumzisha, basi banda zima lisiwe na kuku baada ya kuku wote waliokuwe kuisha.

Acha walau siku 14. Na ndani ya hizi siku, piga dawa mara 2.

👉Tunajua baadhi yetu ufugaji ndo ajira/kazi peke. Hivyo suala la kupumzisha banda linaweza kuwa changamoto!
 *Jambo la msingi ni kujiuliza: Ufuge mfululizo na upate hasara kubwa au upumzishe banda kwa  muda mfupi kuepuka hasara?*

Swali: *Dr nimeshauriwa Duka la mifugo kuchanganya Booster na BIOSPARK V suppliment* Kwa kuku wanapofika wiki ya pili Kwa matokeo mazuri zaidi, sasa nisaidie kuna ukweli wowote hapo au ni Biashara Tu!

 *Jibu:* Hizo 👆 ni Bidhaa mbili tofauti.

 *Biospark* ina 'Amino acids' na madini kidogo

 *Broboost* ina mchanganyiko wa 'Amino acids' Vitamins mbalimbali na madini.

 *Kulingana na uhitaji wako unaweza kutumia moja wapo.* 

Mwisho wa siku, vitu vingine vyote vikiwa sawa, ili kuku wakue vizuri unahitaji *CHAKULA BORA TU* haya mengine ni kujaribu kuziba viraka kwenye mapungufu mbalimbali ndani ya chakula.

Swali: *DR  kwenye vitamin na madawa mengine ya maradhi yanayochanganywa na maji..swala la kutreat maji limekaje.*

JIBU: Hakikisha maji yako hayana vimelea vya magonjwa, haswa bacteria.

Unaweza kutumia

1. Chlorine
2. Hydrogen peroxide
3. Organic acids

Hizi siku hizi zipo madukani.

Ukitumia kwa usahihi, pamoja na kudumisha usafi na chanjo, unaweza kufuga kuku wako bila antibiotics zozote.

Mwisho sio Kwa Faida Muhimu sana, unaweza tumia hata *V-rid* kwenye maji ya kila siku Kwa dose ndogo.

V-rid sio ya kusafishia banda tu 🤓

 *KARIBU TUKUHUDUMIE* 
 *KAHISE POULTRY SOLUTIONS*