❗ *UFUGAJI WA KUKU WA ASILI (KIENYEJI)*❗
Imeandaliwa na
*Greyson Kahise*
*Mtaalamu wa kuku*
_0769799728_
*0715894582*
👆KWA MUDA SASA SIKUWAHI ANDIKA KUHUSU *KUKU WA ASILI* HAPA NAANDIKA BAADHI YA VITU MUHIMU.
👉Kuku wa asili, hawa ni kuku ambao kwetu *Tanzania* tumezoea kuwaita kuku wa kienyeji, na Kuku hawa maeneo mengi hufugwa Kwa Mfumo wa *HURIA*
👆Zipo Aina nyingi za Kuku hawa wa asili kutokana na maeneo tunayo ishi, kama Kuku wa *kisukuma* , *Vishingo* , *Wafupi* , *manyoya yaliyo charuka* , Kuchi, n.k , na Kwa ujumla wake kuku hawa hasa hupatikana maeneo ya *vijijini*
👆 *SIFA KUU ZA KUKU WA ASILI*
👉Wanaatamia ( Kulalia mayai na kuangua).
👉Wanataga Kwa mihula ( *mizunguko 3-4 Kwa mwaka na wengine hata 5* ) Iwapo utawapokonya vifaranga mapema.
👉Wanastahimili magonjwa
👉Wanaweza kutafuta chakula.
👉Baadhi ni mama wazuri (walezi Bora wa vifaranga).
👉Ukuaji wao ni wataratibu
👉Kutaga ni kati ya miezi 6-7 inategemea aina ya chakula.
👆👉Kuku hawa wa asili kwetu Tanzania wafugaji wengi huwafuga Kwa matumizi ya kawaida, na sio kibiashara. Ila wapo wafugaji ambao hufuga kuku hawa Kwa wingi na kuwatumia kama Biashara, *Mfn* : Kuuza mayai, Kuuza vifaranga, Kuuza chakula Chao n.k
*CHANGAMOTO*
👆Shida iliyopo baina ya wafugaji Kwa sasa ni *kujiaminisha* kwamba kwakua kuku hawa ni wa asili basi *hawahitaji* matunzo kama ya kuku Aina nyingine hasa *CHANJO*
👆Mtazamo huu si sahihi, Kwa mana hiyo wanapaswa kupewa chanjo za magonjwa kama wanavofanyiwa kuku Aina nyingine kama *Chotara* , na wale wa *mayai* au *Broilers*
👆 *NAMNA YA KUWAFUGA*
👉Kwa uzoefu kijijini kwetu kiasili kabisa ( Sisi tumejenga Banda la mbao lililo ezekwa Kwa bati, kuku wetu hulala humu usiku, na kila asubuhi huwafungulia kwenda kujitafutia chakula).
👆Wakati wa mchana huwa tunawawekea chakula cha ziada chenye mchanganyiko wa ( *Mahindi paraza, Pumba , Mashudu ya alizeti, mifupa, chokaa* , ) mchanganyiko huu huwasaidia kuku hawa kupata Afya nzuri.
👆 *Chanjo muhimu*
👉Chanjo ya kideri Newcastle ( siku ya 7 na 21)
👉Chanjo ya Gumboro ( Siku ya 14)
👉Chanjo ya Ndui wiki ya 5
👉Dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu.
👆 *TUNAZINGATIA SANA CHANJO KWA SASA* Kwa kuwa kuna msimu tuliwahi na Mzee KAHISE kufuga kuku wakaja Kufa Kwa kideri wote Kwa kuwa hatu kuwachanja *Ipasavyo*
👆 *NB* ! Unaweza tumia vyakula vilivyoboreshwa vya kuku WA kienyeji Kwa matokeo Bora zaidi.
👆👉Kuku hawa pia unaweza *KUWAFUGA* Kwa Mfumo wa *nusu huria* na watakupa matokeo mazuri pia.
*UATAMISHAJI*
👆Kuku hawa wanatofautiana *idadi* ya mayai Kwa Mzunguko *10-20 au zaidi*
👉Hivo baada ya kuku hao kutaga unatakiwa kuwatengenezea kiota ( *Kinaweza kuwa cha majani, Dumu lililokatwa, umetengeneza viota vya mbao, matairi n.k* ) na Utaweka Randa za mbao au Mpunga.
👆 *Utawawekea* kuku wako mayai, na watalalia na kuangua mayai hayo *sharti* Yawe yamerutubishwaa na *JOGOO*
👆👉Ukiangulisha mayai, Anza kulea vifaranga wako
👉Unaweza kuwaacha na mama akawalea, Kwa wiki 2 kisha ukawatenga
👆Unaweza kuwatenga na mama zao mapema kabisa baada ya kuanguliwa
👉Wakianguliwa hakikisha wanapata , joto, chakula , na Vitamins Ipasavyo.
*MFUMO WA ULISHAJI*
👆Starter wiki 1-8
👆Grower wiki 9- watakapo Anza kutaga
👆Layers Wakianza kutaga na kuendelea
🙌 *WAFUGAJI WENGI HULISHA KUKU WA ASILI PUMBA PEKEE,* hii ndio sababu kuku wao huchelewa saana kutaga au *Ukuaji* kuwa wakusua sua Sana).
🐓 *KUKU* wa kienyeji anaweza kuangua mara mbili Mfululizo, akiangua unatoa vifaranga na kuweka mayai mengine ( *Shart chakula na Maji yawepo Jirani).*
*Kuna mambo Mengi Sana ya Kuandika Ila hayo ndio ya msingi na ya kumsaidia MFUGAJI wa kuku wa asili.*
Hii ni Kwa Mujibu wangu *KAHISE* Kwa uzoefu kijijini kwetu pia na *baada ya kujifunza Ufugaji wake sahihi.*

0 Comments